Mkenya Peres Jepchirchir aweka rekodi marathon

Peres Jepchirchir Haki miliki ya picha RAK

Mwanariadha wa Kenya Peres Jepchirchir ameweka rekodi mpya ya dunia katika mbio za half marathon.

Jepchirchir alimaliza mbio hizo kwa muda was aa moja, dakika tano na sekunde sita katika mbio za half marathon za Ras al-Khaimah katika Umoja wa Milki za Kiarabu.

Muda wake ulikuwa sekunde tatu bora ukilinganisha na rekodi ya awali iliyowekwa na Mkenya mwingine Florence Kiplagat mjini Barcelona miaka miwili iliyopita.

Rekodi hiyo hata hivyo bado itahitaji kuthibitishwa na shirikisho la riadha duniani, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Mada zinazohusiana