Mchezaji wa Man United amshukuru Jurgen Klopp

Henrikh Mkhitaryan na Jurgen Klop wakiwa Dortmund Ujerumani Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Henrikh Mkhitaryan na Jurgen Klop wakiwa Dortmund Ujerumani

Kiungo wa kati wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan amemshukuru Jurgen Klop kwa ushauri wake uliomsaidia kuimarika katika timu yake mpya uwanja wa Old Trafford.

Mkufunzi huyo wa Liverpool alimshauri mchezaji huyo wakati mgumu walipokuwa katika klabu ya Borussia Dortmund 2013.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ahsante sana Jurgen Klopp

Mapema msimu huu Mkhitaryan mwenye umri wa miaka 28 hakucheza kwa muda wa wiki 10 na kukumbuka ushauri aliopewa na Klopp.

''Namshakuru sana Klopp'', alinisaidia kiakili'', aliambia BBC.

Raia huyo wa Armenia alihudumu miaka miwili akimchezea Klopp ambaye alijiunga na Liverpool 2015.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkhitaryan akiichezea Manchester United

"Nilipokuwa Dortmund, nilikuwa na shikinizo kubwa la kiakili baada ya kushiriki mechi chache ambapo tulikuwa hatuchezi vyema ,aliongezea Mkhitaryan, ambaye amefunga mara tano msimu huu.

''Klopp alinionyesha njia, alinisaidia na kunambia kutovunjika moyo kwa kuwa ufanisi mkubwa ulikuwa unakuja. Alinisaidia kuwa mchezaji nilivyo''.