Ibrahimovic kimya kuhusu hatma yake Man U

Zlatan Ibrahimovic ameifungia Man U magoli 20 msimu huu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zlatan Ibrahimovic ameifungia Man U magoli 20 msimu huu

Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic amekaa kimya kuhusiana na mkataba wake, licha ya kusema kuwa ametekeleza yote yanayohitajika ili mkataba wake uweze kuongezwa.

Raia huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 35 alijiunga na Man U msimu uliopita kwa mkataba wa mwaka mmoja na tayari amefunga magoli ishirini msimu huu.

Mourinho alisema Ijumaa kuwa striker huyo atasalia Old Trafford mwaka 2017-2018.

Alipouliwa kuhusu hatma yake, Ibrahimovich alisema: "Tutasubiri tuone."

Mabao ya Ibrahimovich yameisaidia Manchester United kufika fainali ya EFL ambapo watakutana na Southampton na pia katika duru ya tano ya kombe FA. Man U pia wako kwenye duru ya maondoano ya Ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zlatan Ibrahimovic