Sadio Mane asababisha mjombake kuvamiwa Senegal

Sadio Mane Haki miliki ya picha Khaled Desouki
Image caption Sadio Mane

Mjomba wake mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane, anasema kuwa anahofia usalama wa familia yake baada ya mpwa wake kukosa penalty na kusababisha Senegal kutimuliwa kutoka mechi ya robo fainali wakati wa mashindano ya Afcon.

Sana Toure alisema kuwa gari ambalo alikuwa amenunuliwa na mpwa wake Mane, ambaye ndiye mchezaji ghali zaidi barani Afrika, liliharibiwa na nyumba yake kulengwa.

"Siku baada la Lions kuondolewa, baadhi ya watu walio na nia mbaya wakataka kuvamia nyumba yangu iliyo Malika. Nawashukuru majirani na wenyeji, kitu kibaya kilizuiwa," Sana Toure alivyambia vyombo vya habari.

Sadio Mane anaonekana kusahau yaliyomsibu Afcom na kufunga mara mbili Liverpool ilipokutana na Tottebnham wikendi hii.