Ngaya ya Comoro yatua Tanzania

Tanzania Haki miliki ya picha Pamoja
Image caption Wachezaji wa timu ya Ngaya ya Comoro watua Tanzania

Kikosi cha timu ya Ngaya kutoka nchini Comoro kimewasili nchini Tanzania kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Yanga katika dimba litakalofanyika mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo imewasili leo saa saba na nusu mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), huku ikiwa imeongozana na baadhi ya viongozi wake.

Mara baada ya kuwasili timu hiyo ilipokelewa na wananchi wa nchi hiyo wanaoishi hapa nchini hata hivyo viongozi wa timu hiyo hawakuwa tayari kuzungumza chochote na wanahabari badala yake walipiga picha ya pamoja na wachezaji na kisha kupanda kwenye magari na kuondoka.

Katika mchezo wa awali uliofanyika nchini humo Yanga iliibuka kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya timu hiyo.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na kuwa waamuzi wake wanatarajiwa kufika kesho.