Mark Clattenburg kuelekea Saudi Arabia

Uingereza
Image caption Mark Clattenburg

Mmoja kati ya maofisa wa ngazi ya juu katika ligi kuu ya Uingereza, Mark Clattenburg, anatarajia kubwaga manyanga ya nafasi yake hiyo na badala yake kuchukua madaraka mapya ya mkuu wa waamuzi au mwite mkuu wa marefa nchini Saudi Arabia.

Mark Clattenburg, tayari amekwisha pangiwa majukumu yake mapya ambayo ni kuhakikisha timu za nchi hiyo zinafanya vizuri na kufanya ligi ya Saudi inakuwa ya kitaalamu zaidi , hata hivyo anatarajiwa pia kuwa msiamamizi mkuu wa baadhi ya michezo ya ligi kuu nchini humo.

Mwaka wa jana, Clattenburg alikuwa muamuzi katika fainali za michuano ya kombe la Ulaya . Wachambuzi wa masuala ya mpira wa miguu wanasema kwa pamoja Saudi Arabia na China hivi karibuni walisajili wachezaji wengi wenye majina makubwa pamoja na makocha kutoka Amerika ya Kusini na Ulaya kwa ujumla, wakitarajia kuinua hadhi ya ligi kuu ya taifa pamoja na wachezaji binafsi ili wafikie viwango vya kimataifa katika mchezo huo.