Mashindano ya ndondi kuwania mkanda wa Commonwealth yakamilika Nairobi

Mashindano ya ndondi ya ambayo yalikuwa ya kusindikiza pigano kati ya Maurice Okolla (Kenya) na Alick Gogodo (Malawi) kuwania mkanda wa Commonwealth katika uzani wa Heavyweight yamekamilika mjini Nairobi katika mkahawa wa Carnivore.

Maurice Okolla alishinda pigano hilo kwa knock out katika raundi ya kwanza

Haki miliki ya picha Peter Njoroge
Image caption Maurice Okolla alixhinda pigano hilo kwa knock out katika raundi ya kwanza

Pigano kati ya Anderson Sifuna kutoka Kenya na Tasha Mjuaji kutoka Tanzania, Sifuna alishinda pingano hili la uzani wa Feather weight kwa wingi wa pointi.

Haki miliki ya picha Peter Njoroge
Image caption Anderson Sifuna kutoka Kenya (kushoto) akipingana na Tasha Mjuaji kutoka Tanzania

Daniel Wanyony alichapana na Karama Nyilawila kutoka Tanzania kwenye uzani wa super Feartherweight

Karama alisalimu amri kwenye roundi ya sita na Daniel Wanyonyi akaibuka mshindi.

Haki miliki ya picha Peter Njoroge
Image caption Daniel Wanyonyi aliibuka mshindi

Pigano kati ya James Onyango kutoka Kenya na Patrick Atuhairwe , uzani wa Welterweight.

Patrick aliaanza kwa mbwembwe na kumlima Onyango konde nzito lililomuamsha simba Onyango.

Dalili zilikuwa wazi kwamba Patrick hatamaliza shindano hili , kwani Onyango aliaaza kumumiminia ngumi nzito nzito.

Patrick alisalimu kwa kulambishwa sakafuni mara mbili.

Haki miliki ya picha Peter Njoroge
Image caption Patrick alisalimu kwa kulambishwa sakafuni mara mbili.

Pigano kati ya bingwa wa dunia wa chama cha WBA uzani wa Light weight, Fatuma Zarika (Kenya) na Flora Machela kutoka Tanzania.

Hii ilikuwa mara ya pili kwa wanandondi hawa kupataka , na ikawa mara ya pili kwa Zarika kushinda Machela.

Haki miliki ya picha Peter Njoroge
Image caption Pigano kati ya Fatuma Zarika (Kenya) na Flora Machela kutoka Tanzania.

Ilichukwa muda chini ya dakika mbili nukta kumi na tano kwa Zarika kumaliza kazi kwa njia ya KO.

Flora Machela aliangushwa sakafuni kutokana na konde kali kutoka kwa Zarika.

Haki miliki ya picha Peter Njoroge
Image caption Flora Machela akiwa sakafuni

Fatuma Zarika alitangazwa mshindi wa pigano hilo.

Haki miliki ya picha Peter Njoroge
Image caption Zarika alitangazwa mshindi

Pigano kati ya David Rajuli kutoka Afrika kusini na Cosmas Cheka kutoka Tanzania.

Haki miliki ya picha Peter Njoroge
Image caption David Rajuli (kushoto),kutoka Afrika kusini na Cosmas Cheka kutoka Tanzania.

Cheka, alionyesha mchezo mzuri sana.Huku akiondokea mashambulizi ya Rajuli kwa ustaandi.

Kwenya roundi ya sita Rajuli alionekana kuwa na macho mekundu sana na mwamuzi alisimamisha pingano hilo.

Haki miliki ya picha Peter Njoroge
Image caption Refa alisimamisha pigano