Manchester city yabanwa na Stoke city-EPL

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mchezaji wa Manchester City

Klabu ya soka ya Manchester city wakiwa nyumbani Etihad imelazimishwa sare tasa na Stoke city katika mchezo pekee wa ligi kuu England uliopigwa jana usiku kufuatia matokeo ya bila kufungana (0-0).

Manchester city bado imebakia katika nafasi ya tatu nyuma ya Tottenham kwa alama 56 kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Ligi kuu ya England inatarajia kuendelea tena machi 11 kwa michezo mitatu,Bornemouth watawakaribisha West Ham United,Evertonni wenyeji wa West Bromwich Albion na Hully city watakuwa wenyeji wa Swansea city.