Mashabiki wavuruga mechi kati ya Senegal na Ivory Coast

Mashabiki wavuruga mechi kati ya Senegal na Ivory Coast Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mashabiki wavuruga mechi kati ya Senegal na Ivory Coast

Mechi ya kirafiki kati ya Ivory Coast na Senegal ilisimamishwa wakati mashabiki waliingia uwanjani mjini Paris.

Timu hizo kutoka Afrika zilikuwa sare ya bao moja dakika ya 88, wakati mashabiki wachache waliingia uwanjani huku mmoja akionekana akimrukia mchezaji wa Senegal Lamine Gassama.

Wachezaji walitoka kutoka uwanajania na refa Tony Chapron akaamua kusimamisha mechi hiyo.

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane alikuwa ameipa Senegal bao la kwanza mnamo kipindi cha pili, lakini Bi Gohi Cyriac akasawazisha dakika tatu baaadaye.

Mwandishi wa habari wa shirika la L'Equipe Herve ambaye alikuwa uwanjani wakati huo aliambia BBC kuwa kisa hicho kingekuw kibaya.

"Sitaweza kusema kuwa watu hao walikuwa na ghasia, lakini ni kama walikuwa wanajaribu kuwafikia wachezaji," mwandishi huyo aliongeza.

Hii ndiyo mara ya pili ndani ya miaka mitano mechi kati ya chi hizo imesimamishwa kutokana na vurugu za mashabiki.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mashabiki wavuruga mechi kati ya Senegal na Ivory Coast