Wenger: Nimepanga wachezaji nitakaonunua

Arsene Wenger na wachezaji wake
Image caption Arsene Wenger na wachezaji wake

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa ameanza kupanga kuhusu wachezaji atakaonunua msimu ujao licha ya kuwa hajapata thibitisho kwamba atasalia katika klabu hiyo.

Kandarasi ya Wenger inaisha mwisho wa msimu huu na tayari amepewa kandarasi mpya ya miaka miwili, ijapokuwa hajatangaza iwapo ataendelea au la.

''Nafanya kazi hadi siku ya mwisho ya msimu'', alisema Wenger mwenye umri wa miaka 67.

''Wachezaji wanaonunuliwa ndio mpango wa kila klabu katika siku zake za usoni'' ,alisema Wenger.

''Swala la iwapo nitasalia au la sio muhimu kwa sasa, kilicho muhimu ni siku za usoni za klabu hii'',Wenger alisema mnamo mwezi Februari kwamba ataamua kuhusu kandarasi mpya mnamo mwezi Machi ama Aprili na baadaye kutangaza.

''Najua nitakachofanya na hivi karibuni mutajua''.