Chelsea yafuta ziara yake Manchester kufuatia shambulizi la Jumapili

Chelsea walikabidhiwa kombe la ubingwa siku ya Jumapili katika uwanja wa Stamford Bridge
Image caption Chelsea walikabidhiwa kombe la ubingwa siku ya Jumapili katika uwanja wa Stamford Bridge

Klabu ya soka ya Chelsea imefuta ziara ya kulitembeza kombe la EPL mjini Manchester baada ya shambulizi la siku ya Jumapili wakati wa utumbuizaji wa muziki.

Klabu hiyo imesema kuwa haitakuwa jambo jema kuwafanya watu warundikane kwa wakati huu ambao ulinzi umeimarishwa mjini Manchester.

Chelsea imepanga kutumia basi la wazi kulitembeza kombe hilo Uingereza na iwapo watafanikiwa kushinda la FA dhidi ya Arsenal siku ya Jumamosi watajumuisha yote.

Wachezaji wa Chelsea kwa pamoja watatoa michango yao kwa wahanga.

Pia watavaa vitambaa vyeusi siku ya mchezo wa fainali ya FA Jumamosi watakapochuana na Arsenal.