Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 16.08.2017 na Salim Kikeke

Serge Aurier Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Serge Aurier

Chelsea wanajiandaa kutoa pauni milioni 50 kumsajili beki wa Tottenham Danny Rose, 27, baada ya mchezaji huyo kushutumu sera za usajili za Spurs. (Sun)

Tottenham wamefikia makubaliano na PSG kumsajili beki Serge Aurier, 24, ambaye alikuwa akifuatiliwa na Manchester United. (L'Equipe)

Tottenham wana uhakika wa kukamilisha usajili wa beki wa kati wa Ajax, Davinson Sanchez, 21, kwa pauni milioni 27. (Daily Mirror)

Dau la Chelsea la kumtaka beki Alex Sandro, 26, limekataliwa na Juventus. (Daily Mail)

Meneja wa Chelsea anataka Alex Sandro awasilishe maombi ya kuondoka Juventus baada ya dau la pauni milioni 52 na 61 kukataliwa. (London Evening Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alex Sandro

Chelsea sasa wamemgeukia beki Cedric Soares, 25, wa Southampton. (Telegraph)

Kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain anataka pauni 150,000 kwa wiki ili kujiunga na Chelsea. (Goal)

Chelsea wanajaribu kumsajili mshambuliaji wa Torino Andrea Belotti, 23, kuziba nafasi ya Diego Costa. (Daily Star)

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema klabu yake itakataa dau lolote la kumtaka Alexis Sanchez, 28, na Alex Oxlade-Chamberlain, na anatarajia wawili hao kuheshimu mikataba yao. (Daily Mirror)

Liverpool wanataka kiungo Ivan Rakitic, aunganishwe kwenye mkataba wa Barcelona kumsajili Philippe Coutinho. (Diario Gol)

Juventus wanamtaka kiungo wa Manchester United Marouanne Fellaini, 29. (Sun)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ivan Rakitic

Real Madrid wapo tayari kuwazidi kete Tottenham na kumsajili beki wa Ajax Davinson Sanchez. (Don Balon)

Manchester City sasa wamemgeukia Eden Hazard wa Chelsea baada ya kubadili mawazo ya kumtaka Alexis Sanchez. (Don Balon)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza): Uhamisho wa wachezaji Ulaya

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na wiki njema.

Mada zinazohusiana