Tetesi za soka Ulaya Jumapili 20.08.2017 na Salim Kikeke

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danny Drinkwater

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anapanga kutumia pauni milioni 200 kuwasajili Danny Drinkwater, 27, kutoka Leicester, kiungo wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain, 24, na mabeki watatu wa Southampton, Virgil Van Dijk, 26, Cedric Soares, 25, na Ryan Bertrand, 28. (Express)

Chelsea wamemuulizia beki wa kati wa Tottenham Toby Alderweireld, 28, ambaye mazungumzo yake na Spurs kuhusu mkataba mpya yanasuasua. (Sunday Times)

Baada ya kumkosa Danny Drinkwater, meneja wa Chelsea sasa atamgeukia Grzegorz Krychowiak wa PSG. (Sun)

Atletico Madrid wapo tayari kutoa pauni milioni 50 kumsajili Diego Costa kutoka Chelsea. (Daily Mail)

Diego Costa amekataa kwenda kwa mkopo katika timu za SIPG na Tianjin Quanjian za China ambapo angelipwa pauni milioni 13 kati ya sasa hadi mwezi Novemba. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Diego Costa

Manchester City wapo tayari kuilipa Arsenal pauni milioni 70 ili kumsajili Alexis Sanchez, 28. (Mirror)

Manchester City watampa Alexis Sanchez, mshahara wa pauni 400,000 na kumfanya mchezaji anayelipwa zaidi England. (Sun on Sunday)

Barcelona watalipa pauni milioni 36.5 za kutengua kipengele cha uhamisho cha Jean Michel Seri, 26, na huenda wakakamilisha usajili wake ifikapo Jumatatu kutoka Nice. (Mundo Deportivo)

Barcelona wamewaambia Liverpool wana hadi siku ya Jumapili kukubali au kukataa dau la pauni milioni 118 la kutaka kumsajili Philippe Coutinho, 25, vinginevyo dau hilo litaondolewa mezani. (Times)

Barcelona wameweka usajili wa Philippe Coutinho kuwa kipaumbele na wanafanya kila jitihada kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil. (Sport)

Haki miliki ya picha PA
Image caption Philippe Coutinho

Barcelona watapanda dau jipya la pauni milioni 130, ingawa Liverpool wanasema thamani ya Philippe Coutinho ni pauni milioni 140. (Express)

Luis Suarez amewaambia Barcelona kuwa kumsajili Philippe Coutinho "sio dawa" ya matatizo waliyonayo sasa hivi. (Liverpool Echo)

Paris Saint-Germain hatimaye wamefikia makubaliano na Monaco ya kumsajili Kylian Mbappe, 18, kwa pauni milioni 182. (Mundo)

Newcastle wanafikiria kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll, 28. (Mirror)

Manchester United, Arsenal na Liverpool zinamtaka Julian Draxler, 23, wa PSG. (Mirror)

Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc amesema mshambuliaji Ousmane Dembele atauzwa kwa bei inayofaa. (FourFourTwo)

Image caption Ousmane Dembele

Barcelona watalazimika kutoa pauni milioni 137 pamoja na marupurupu juu ikiwa wanataka kumsajili Ousmane Dembele, 20. (RAC 1)

Arsenal wamewapa AC Milan nafasi ya kumsajili kiungo Jack Wilshere. (Corriere dello Sport)

Real Madrid wamekataa dau la pauni milioni 68.5 kutoka kwa Juventus kutaka kumsajili Mateo Kovacic, 23. (AS)

Arsenal, Tottenham na Manchester City wanataka kumsajili kiungo wa Fenerbahce Oguz Kagan, 18. (Sun)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumapili njema.