Chelsea wamsajili Drinkwater kutoka Leicester

Danny Drinkwater Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danny Drinkwater alicheza mechi 35 na kuwasaidia Leicester kushinda Ligi ya Premia 2015-16

Chelsea wamemnunua kiuungo wa kati Danny Drinkwater kutoka Leicester City kwa £35m.

Mchezaji huyo wa miaka 27 alichangia sana katika kikosi cha Leicester kilichoshinda Ligi ya Premia msimu wa 2015-16 lakini aliomba kuihama klabu hiyo baada ya kutambua kwamba atafutwa na Chelsea.

Chelsea pia wamemnunua beki Davide Zappacosta kutoka Torino kwa mkataba wa miaka minne kwa ada ambayo haijafichuliwa.

Hata hivyo, mshambuliaji Fernando Llorente ameamua kwenda Tottenham badala ya Stamford Bridge.

Na kiungo wa kati wa Everton Ross Barkley alibadilisha nia yake kuhusu kuhamia katika klabu hiyo ya Antonio Conte.

Leicester wanatarajia kumsajili Adrien Silva, 28, kutoka Sporting siku ya Ijumaa kwa £22m kujaza nafasi ya Drinkwater.

Kiungo huyo wa kati alicheza mechi 35 kati ya 38 Ligi ya Premia msimu ambao Leicester walishinda ligi na alikuwa na ushirikiano mzuri na N'Golo Kante, ambaye alijiunga na Chelsea Julai mwaka jana.

Bado hajacheza mechi hata moja msimu huu kutokana na jeraha la misuli yapaja.

Kiungo huyo wa kati alijiunga na leciester mwaka 2012 akitokea Manchester United, na amechezea timu ya taifa ya England mechi tatu tangu awachezee mara ya kwanza Machi 2016.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zappacosta alianza uchezaji wake katika ligi ya daraja ya nne Italia, klabu ya Isola Liri

"Nina furaha sana kuwa mchezaji wa Chelsea na nasubiri sana kuanza kucheza," amesema Drinkwater.

"Imekuwa safari ndefu kufika hapa, lakini nina furaha na nasubiri kuisaidia klabu hii kushinda vikombe zaidi.

Zappacosta amechezea timu ya taifa ya Italia mara nne na Conte ndiye aliyemchezea mara ya kwanza Mei 2016.

Mchezaji huyo wa miaka 25 alijiunga na Torino kutoka Atalanta mwaka 2015 na alicheza mechi 29 katika Serie A msimu uliopita.

Mada zinazohusiana