Tetesi za soka Ulaya Jumanne 05/09/2017

Gareth Bale
Image caption Gareth Bale

Klabu ya Manchester United itawasilisha ombi jingine la mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale ,28, msimu ujao huku Jose Mourinho akitafuta kusamjili winga maarufu duniani (Sun)

Tottenham italazimika kumpatia beki wa kati Toby Alderweireld, 28, mapato mapya yalioimarika ama imwachilie kuhamia klabu nyengine kulingana na mshauri wa mchezaji huyo. (Het Nieuwsblad via Daily Telegraph)

Image caption Kiungu wa kati wa Chelsea Eden Hazard amemtaka mshambuliaji Diego Costa kutafuta suluhu ya kuhakikisha kuwa ataichezea tena klabu hiyo

Kiungu wa kati wa Chelsea Eden Hazard amemtaka mshambuliaji Diego Costa kutafuta suluhu ya kuhakikisha kuwa ataichezea tena klabu hiyo.Costa mwenye umri wa miaka 28 hajaichezea timu hiyo msimu huu baada ya kukataa kurudi katika mazoezi. (Marca via Daily Mirror)

Arsenal inajaribu kuanzisha mazungumzo ya kandarasi za wachezaji ambao mikataba yao inakamilika mwisho wa msimu ujao ili kuzuia tatizo kama lile la msimu huu ambapo wachezaji kama vile Alexis Sanchez na Mesut Ozil walianza msimu wakiwa wamesalia na kandarasi ya mwaka mmoja kila mmojawao. (Daily Telegraph)

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Arsenal Ivan Gazidis amewatumia ujumbe wachezaji wa timu hiyo akiwaambia kwamba kikosi chao kilichoimarika kinaweza kugombea taji la Uingereza msimu huu.

Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Arsenal Ivan Gazidis amewatumia ujumbe wachezaji wa timu hiyo akiwaambia kwamba kikosi chao kilichoimarika kinaweza kugombea taji la Uingereza msimu huu.(Daily Star)

Mkufunzi wa Celtic Brendan Rodgers anasema kuwa klabu hiyo itakuwa imevunja rekodi yake ya uhamisho itakapomsajili Patrick Robert kwa kandarasi ya kudumu lakini Manchester City haitaki kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kwa kitita cha £30m. (Goal)

Haki miliki ya picha iStock
Image caption Manchester United sio klabu isiojulikana iliowasilisha ombi la kutaka kumsajili winga wa Leicester Riyadh Mahrez mwenye umri wa miaka(Leicester Mercury)

Manchester United sio klabu isiojulikana iliowasilisha ombi la kutaka kumsajili winga wa Leicester Riyadh Mahrez mwenye umri wa miaka(Leicester Mercury)

Kiungo wa kati wa Everton Ross Barkley hakujiunga na Chelsea katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho kwa sababu simu ya mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte ilipuuziliwa mbali wakati mwakilishi wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alipotaka kuzungunmza jukumu lake kulingana na mchezaji wa zamani wa Manchester CityJoey Barton. (Talksport)

Winga wa Everton Kevin Mirallas mwenye umri wa miaka 29 amekasirika baada ya klabu hiyo kumkataza kurudi klabu yake ya zamani Olympiakos (Daily Mirror)

Juventus iko tayari kumnunua beki wa Napoli Faouzi Ghoulam ambaye amevivutia vilabu vya Chelsea na Liverpool (Tuttosport via Talksport)

Image caption Leicester City huenda wasimsajili beki wa kulia wa Manchester City Bacary Sagna licha ya kushirikishwa na klabu hiyo kama ajenti huru.(Leicester Mercury)

Leicester City huenda wasimsajili beki wa kulia wa Manchester City Bacary Sagna licha ya kushirikishwa na klabu hiyo kama ajenti huru.(Leicester Mercury)

Kinda wa kimataifa wa Uhispania Arnau Puigmal ,mwenye umri wa miaka 6, amejiunga na Manchester United kutoka Espanyol (Manchester Evening News)

Juventus inajiandaa kuwasajili wachezaji watatu wa kiungo cha kati wakati kandarasi zao zitakapokamilika msimu ujao.

Klabu hiyo ya ligi ya Serie A inamtaka mchezaji wa Bareclona Andres Iniesta, 33, mchezaji wa Liverpool Emre Can, 23, na mchezaji wa Schalke's Leon Goretzka, 22. (Tuttosport via 90min)