Manvir Singh atamba katika mashindano ya magari Rwanda

Manvir Singh
Image caption Mkenya Manvir Singh anahitaji alama 25 za shindano hili la Rwanda ili kutangazwa bingwa wa Afrika

Mashindano ya mbio za magari ya Rwanda mountain Rally yanaendelea huku dereva kutoka Kenya Manvir Singh akiendelea kutamba.

Manvir Singh akiendesha gari lake aina ya skoda ameshinda awamu zote zilizochezwa leo asubuhi na kujiweka katika nafasi nzuri ya kunyakua ubingwa wa mashindano haya hata kutwaa taji la afrika.Magari 10 ndiyo yamesalia katika mashindano hayo yaliyoanza Ijumaa yanayoshirikisha washindani 16.

Gari hilo aina ya Skoda ndiyo gari ya kisasa miongoni mwa magari yanayotumiwa katika mashindano ya mbio za magari bei yake ikiwa ni 280.000 USD kulingana na Dereva huyo.

Dereva huyo kutoka Kenya Manvir Singh akiwa anahitaji alama 25 za shindano hili la Rwanda ili kutangazwa bingwa wa Afrika kabla hata ya shindano la mwisho litakalofanyika Zambia.

Mbio za Jumamosi ni za urefu wa km 140 zikizunguka katika barabara mbovu za upande wa kusini mashariki mwa Rwanda.

Jumla ya magari 16 yameshiriki mashindano haya ya siku tatu.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii