Bondia Jake LaMotta afariki akiwa na miaka 95

LaMotta alikuwa mpiganaji na mchekeshaji
Image caption LaMotta alikuwa mpiganaji na mchekeshaji

Bondia wa zamani wa uzito wa kati na mchekeshaji Jake LaMotta,amefariki dunia akiwa na miaka 95.

Mke wake amesema LaMotta amefariki nyumbani kwake kwa ugonjwa wa homa ya mapafu.

Alikuwa mpiganaji maarufu zaidi miaka ya 40 na 50.

Image caption LaMotta enzi za upiganaji

Atakumbukwa kwa uvaaji wa kaptula yenye mistari ya chuichui na wakati fulani alikua akiingiza uchekeshaji wakati akipigana jambo lililomfanya mpinzani wake kuishia kucheka na yeye kushinda.