Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 23.09.2017

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ameanza harakati za kutaka kusaini kandarasi mpya na Aaron Ramsey na Danny Welbeck
Image caption Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ameanza harakati za kutaka kusaini kandarasi mpya na Aaron Ramsey na Danny Welbeck

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ameanza harakati za kutaka kusaini kandarasi mpya na Aaron Ramsey na Danny Welbeck akiongezea kuwa anatarajia wachezaji wengine kukamilisha kandarasi zao. Kandarasi za wawili hao zinakamilika 2019.(Guardian)

Real Madrid wanamchunguza mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane kwa lengo la kumsajili via Daily Express)

Image caption Real Madrid wanamchunguza mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane kwa lengo la kumsajili via Daily Express)

Chelsea inaongoza Liverpool, Tottenham, Southampton, Manchester City na Manchester United katika kumsaka kinda Elye Wahi, 14, ambaye tayari ameanza kuifungia klabu ya Caen ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 na anatoka katika mtaa wa Courcouronnes, makaazi ya Paris ambayo kiungo wa kati wa Chelsea N'Golo Kante anatoka. (Sun)

Arsenal wana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Napoli Dries Mertens, 30, msimu huu wa joto wakitumia fursa ya mchezaji huyo kuwa huru baada ya malipo ya £26.5m katika kandarasi yake (Calciomercato)

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Andy Caroll

Mkufunzi wa West Ham Slaven Bilic anasema kuwa mshambuliaji Andy Carroll, 28 ambaye amesalia na miaka miwili katika kandarasi yake na West Ham ni sharti aonyoshe kwamba anaweza kushiriki katika mechi iwapo anahitaji mkataba mpya.(Daily Mail)

Uwezekano wa winga wa Paris St-Germain Julian Draxler, 24, kuhamia katika ligi ya Uingereza mwezi Januari umegonga mwamba.. (Daily Star)

Rais wa Real Madrid Florentino Perez amemwambia mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho kumsajili kiungo wa kati Andre Gomes, 24, kutoka klabu ya Barcelona msimu ujao (Don Balon - in Spanish)

Image caption Gabriel Jesus kuongezwa mshahara Manchester City

Mshambualiji wa Manchester City Gabriel Jesus, 20, anatarajiwa kupewa nyongeza ya mshahara baada ya kuanza majadiliano kuhusu kandarasi mpya miezi tisa baada ya uhamisho wake wa £27m kutoka klabu ya Palmeiras. (Manchester Evening News)

Kiungo wa kati Ruben Loftus-Cheek, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Crystal Palace kutoka Chelsea, anasema kuwa hajui kuhusu hatma yake na Chelsea. (Daily Star)

Image caption Mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang, 28, amesema kuwa hakutaka kuondoka Borussia Dortmund ili kujiunga na ligi ya China. (Daily Mail)

Mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang, 28, amesema kuwa hakutaka kuondoka Borussia Dortmund ili kujiunga na ligi ya China. (Daily Mail)

Real Madrid wanafanya mazungumzo ya kutaka kumsajili kipa wa Athletic Bilbao Kepa Arrizabalaga. (Don Balon - in Spanish)

Beki wa kushoto wa klabu ya Manchester City Benjamin Mendy, 23, amesema kuwa mchezaji mwenza wa zamani Kylian Mbappe, 18, Tiemoue Bakayoko, 23, na Bernardo Silva, 23, walikubaliana kwamba watatuma picha zao wakati watakaposaini na klabu mpya msimu huu.

Mada zinazohusiana