Arsenal wageni wa BATE Borisov - Europa League

Arsenal wageni wa BATE Borisov Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsenal wageni wa BATE Borisov

Michuano ya Uefa Europa League inatarajiwa kuchezwa hii Leo kwa michezo kadhaa ikiwa ni hatua ya Makundi, miongoni mwa michezo ambayo inatazamiwa kuchezwa BATE Borisov wanacheza na Arsenal, Salzburg dhidi ya Marseille, Zenit wanawakaribisha Sociedad, Everton ni wenyeji wa Apollon, Locomotiv watakuwa ni wenyeji wa Fastav, Maccabi Tella Viv wanawaalika Vilareal , Lyon inamenyana na Atalanta .

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsene Wenger

FC Astana ni wenyeji wa Slavia Prague, Partizan Beograd wanawaalika Dynamo Kyiv, Skenderbeu ni wenyeji wa Young Boys, FC Cologne watamenyana na FK Crvena Zvezda, AC Milan ni wenyeji wa Rijeka.