Nchi tatu zataka kuchukua nafasi ya Kenya kuandaa mechi za CHAN

Equitorial Guinea, Ethiopia na Morocco watuma maombi ya kuandaa mechi za CHAN Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Equitorial Guinea, Ethiopia na Morocco watuma maombi ya kuandaa mechi za CHAN

Shirikisho la kandanda barani Afrika (Caf) limethibitisha kuwa Equitorial Guinea, Ethiopia na Morocco wametuma maombi ya kuandaa mechi za taifa bingwa barani Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN).

Morocco ilithibitisha ombi lao siku ya Jumamosi, nao Caf wakatangaza jana Jumapili kuwa pia kulikuwa na maombi kutoka nchini Ethiopia na pia Equitorial Guinea, ambao waliandaa mechi za taifa bingwa barani Afrika mwaka 2015.

Caf wanatafuta mwandalizi mpya kuchukua mahala pa Kenya ambayo ilipoteza fursa hiyo baada ya kushindwa kutimiza matakwa ya shirikisho la Caf

Sasa yule ambaye atapata fursa ya kuandaa mechi hizo ambazo huandaliwa kila baada ya miaka mwili waka wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani atatangazwa wiki ijayo.

Mechi hizo zinatarajiwa kuandaliwa kuanzia Januari 12 na Februari 4 mwaka 2018.

Mada zinazohusiana