Rushwa yamponza Carlos Nuzman

Olimpic Haki miliki ya picha Empics
Image caption Carlos Nuzman Kiongozi wa Olimpiki kutoka Brazil akiwa mikononi mwa polisi huko Rio

Polisi wamemkamata kiongozi wa kamati ya Olimpiki kutoka nchini Brazil kwa tuhuma za kujihusisha na masuala ya rushwa.

Waendesha mashitaka wa Brazil wamemtaja bwana Carlos Nuzman kuwa ndiye muhusika na kwamba aliendesha harakati za kutoa rushwa ili wajumbe wahakikishe Rio de Janeiro inapata haki ya kuwa mwenyeji wa michuano ya Olimpiki ya mwaka 2026.

Waendesha mashitaka hao wameendelea kueleza kuwa mpango huo ulikuwa na baraka za mkurugenzi wa zamani wa jiji la Rio Sergio Cabral, ambaye yuko jela kutokana na madai ya rushwa na pia kosa la utakatishaji fedha.

Bwana Nuzman amekana tuhuma zote zinazomkabili.

Naye mwanasheria wake ameelezea kukamatwa kwa mteja wake kama kusikokuwa na umuhimu, na kwamba ni kinyume cha sheria.

Mwezi uliopita nyumba ya bwana Nuzman ilipigwa mnada na mali zake zilizuiliwa.