Ujerumani yafuzu kwa Kombe la Dunia 2018

Germany walihitaji kutoka sare au kushinda kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 Haki miliki ya picha Press Eye
Image caption Germany walihitaji kutoka sare au kushinda kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018

Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia Ujerumani wamefuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Urusi baada ya kulaza Ireland Kaskazini 3-1 mjini Belfast.

Sebastian Rudy alifunga bao dakika ya pili, Sandro Wagner akaongeza la pili baadaye, naye Joshua Kimmich akafunga la tatu mechi ikikaribia kumalizika.

Josh Magennis alifungia Ireland Kaskazini bao la kufutia machozi kwa kutumia kichwa dakika za lala salama.

Ujerumani wamefuzu wakiwa viongozi wa kundi lakini Ireland Kaskazini wanasalia bado na matumaini ya kufuzu kupitia mechi za muondoano za kufuzu Novemba.

Vijana hao wa Michael O'Neill watamaliza mechi zao Kundi C nchini Norway Jumapili, wakilenga kumaliza wakiwa miongoni mwa timu nane bora zitakazomaliza nafasi ya pili kati ya makundi tisa ya kufuzu.

Haki miliki ya picha Press Eye
Image caption Mshambuliaji wa Charlton Josh Magennis alifunga bao dakika ya mwisho kabisa

Huenda wakahitaji alama moja Oslo kufika mechi za kufuzu za muondoano.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ireland Kaskazini wameshindwa mechi zao mbili kundini mikononi mwa Ujerumani

Droo ya mechi hizo itafanyika tarehe 17 Oktoba.

Mada zinazohusiana