Andrea Iniesta atia saini kandarasi ya maisha na Barcelona

Lionel Messi na Andrea Iniesta Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lionel Messi na Andrea Iniesta

Kiungo wa kati wa Barcelona na nahodha Andres Iniesta ametia saini kandarasi ya maisha na mabingwa hao wa Ulaya.

Mchezaji huyo wa Uhispania ,33, ameichezea Barcelona mara 639 ikiwa na wa pili kushiriki mechi nyingi na timu hiyo na kufunga mabao 55.

Iniesta alikuzwa na shule ya magfunzo ya soka ya Barcelona kwa jina La Masia baada ya kujiunga akiwa na umri wa miaka 12.

Alishiriki mechi yake ya kwanza mnamo mwezi Oktoba 2002 na amefanikiwa kushinda mataji 8 ya ligi ya Uhispania na makombe manne ya vilabu bingwa Ulaya.

Iniesta anekuwa nahodha wa timu hiyo tangu 2015 na anagawana rekodi ya kushinda mataji mengi na Lionel Messi kwa kushinda mataji 30 katika historia ya Berclona.

Ameshinda kombe la Yuro mara mbili na Uhispania na kuweza kufunga bao la dakika za lala salama katika kombe la dunia la 2010 dhidi ya Uholanzi nchini Afrika Kusini.

Taarifa ya klabu inasema: Andres Iniesta ametia saini kandarasi ya maisha na Barcelona siku ya Ijumaa katika makubaliano ambayo yatamuweka katika klabu hiyo kwa maisha yake yote ya soka.

Mchezaji huyo wa Uhispania ,33, ameichezea Barcelona mara 639 ikiwa ni wa pili kushiriki mechi nyingi na timu hiyo na kufunga mabao 55.

Iniesta alikuzwa na shule ya mafunzo ya soka ya Barcelona kwa jina La Masia baada ya kujiunga akiwa na umri wa miaka 12.

Alishiriki mechi yake ya kwanza mnamo mwezi Oktoba 2002 na amefanikiwa kushinda mataji 8 ya ligi ya Uhispania na makombe manne ya vilabu bingwa Ulaya.

Iniesta amekuwa nahodha wa timu hiyo tangu 2015 na anagawana rekodi ya kushinda mataji mengi na Lionel Messi kwa kushinda mataji 30 katika historia ya Berclona.

Ameshinda kombe la Yuro mara mbili na Uhispania na kuweza kufunga bao la dakika za lala salama katika kombe la dunia la 2010 dhidi ya Uholanzi nchini Afrika Kusini.

Taarifa ya klabu inasema: Andres Iniesta ametia saini kandarasi ya maisha na Barcelona siku ya Ijumaa katika makubaliano ambayo yatamuweka katika klabu hiyo kwa maisha yake yote ya soka.

Mada zinazohusiana