Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 10.10.2017

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danny Rose

Manchester United wana matumaini ya kumsajili mlinzi wa Tottenham Danny Rose,27, mwezi Januari (Tuttomercato, via Talksport)

Barcelona wanajitahidi kumpata mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, kwa pauni milioni 89 kabla ya thamani ya mchezaji huyo wa umri wa miaka 26 kupanda msimu ujao (Mundo Deportivo, via Daily Mirror)

Paris St-Germain wako katika mikakati ya kumuuza wing'a Angel di Maria, 29, kwenda China mwezi Januari.(TMW, via Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Angel di Maria

Arsenal wameafikia makubaliano na wing'a wa zamani Marc Overmars,44, ya yeye kuondoka Ajax na kuwa mkurugezi wa kandanda kuanzia msimu ujao.(Tuttomercato, via Daily Express)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa zamani wa Italia Andrea Pirlo, 38, hajakana mpango wa kujiunga na kikosi cha makocha, kufuatia uamuzi wake wa kustaafu misho wa msimu wa MLS. (Gazzetta dello Sport, via London Evening Standard)

Meneja wa Manchetser United Jose Mourinho alikuwa ndani umati wakati wa ushindi wa Austria dhidi ya Serbia, kumtazama wing'a wa Eintracht Frankfurt, Mijat Gacinovic, 22. (Daily Mirror)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Aleksandar Mitrovic

Mshambuliaji Newcastle Aleksandar Mitrovic, 23, ananyemelewa na Brighton hapo Januari. (Daily Mirror)

Everton wanammezea mate mshambuliaji wa Sporting Lisbon Bas Dost. Mchezaji huyu wa umri wa miaka 28 amefunga mabao 36 kwa mechi 41 kwa klabu hiyo ya Ureno. (ESPN)

Mlinzi wa Manchester United Daley Blind 27, anawindwa na Galatasaray ya Uturuki (Calciomercato, via Talksport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Harry Winks

Tottenham ilikataa ombi na Nice ya Ufaransa kumnunua mchezaji wa kiungo cha kati Harry Winks,21, kwa mkopo msimu uliopita. (Daily Mail)

Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 31, amethibitisha kuwa nusura ajiunga na Everton msimu uliopita. (Canal Plus, via Sky Sports)