Sergio Aguero: Nyota wa Man City arejea mazoezini baada ya ajali

Sergio Aguero Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sergio Aguero amefungia Manchester City mabao 176 - amepungukiwa na moja tu kufunga rekodi

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero amerejea mazoezini siku 11 baada yake kuvunjika ubavu katika ajali ya barabarani mjini Amsterdam.

Aguero, 29, alikuwa ametarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki kadha

Hata hivyo, alirejea kufanya mazoezi mepesi Jumanne.

City wamesema mchezaji huyo wa Argentina ataendelea "kuimarisha hali yake ya mwili siku zijazo akilenga kurejea kikosini".

Aguero anahitaji bao moja pekee kufikia rekodi ya ufungaji mabao City ya Eric Brook ambayo ni mabao 177.

City wanaongoza Ligi ya Premia kwa wingi wa mabao, mbele ya Manchester United, na watakutana na Stoke siku ya Jumamosi.

Aguero alijeruhiwa akiwa kwenye teksi akisafiri baada ya kuhudhuria tamasha ya muziki. Teksi hiyo iligonga boriti ya taa barabarani.

Alikuwa ameenda Amsterdam kumuona nyota wa muziki kutoka Colombia Maluma akitumbuiza.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii