Ureno na Ufaransa zafuzu Kombe la Dunia Urusi 2018

Portugal goal Haki miliki ya picha EPA

Mabingwa wa Ulaya Ureno walilaza Uswizi 2-0 Jumanne mjini Lisbon na kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi kwa kumaliza kileleni Kundi B.

Iwapo wangeshindwa au kutoka sare, basi wangehitaji kucheza mechi ya muondoano kufuzu.

Lakini mabao mawili, moja la Johan Djourou aliyejifunga na Andre Silva, yalitosha kuwavusha Ureno.

Ufaransa walilaza Belarus 2-1 nakufuzu kwa kumaliza kileleni Kundi A, Sweden nao wakamaliza wa pili licha ya kushindwa 2-0 na Uholanzi.

Waholanzi ambao walimaliza nafasi ya tatu Kombe la Dunia 2014 wameondolewa kwenye michuano hiyo.

Walihitaji kushinda kwa mabao saba ya wazi kuwapiku Sweden na kumaliza wa pili.

Walifunga mabao mawili pekee kuptiia Arjen Robben.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ureno walifunga mabao 32 mechi zao 10 za kufuzu kwa Kombe la Dunia
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mabao ya Olivier Giroud (pichani) na Antoine Griezmann yaliwapa Ufaransa ushindi wa 2-1 dhidi ya Belarus

Kundi H, Ugiriki walijihakikishia nafasi michezo ya muondoano kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya Gibraltar.

Ubelgiji ambao tayari walikuwa wamejihakikishia uongozi katika kundi hilo walilaza Cyprus 4-0 huku nyota wa Chelsea Eden Hazard akifunga mabao mawili, nduguye Thorgan akafunga moja naye mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku akafunga ukurasa wa mabao.

Mataifa ya Ulaya ambayo yamefuzu kwa sasa ni Ufaransa, Ureno, Ujerumani, Serbia, Poland, England, Uhispania, Ubelgiji na Iceland.

Kuna nafasi nne zaidi za kushindaniwa na mataifa manane kupitia muondoano wa timu nane - Sweden, Uswizi, Ireland Kaskazini, Jamhuri ya Ireland, Denmark, Italia, Ugiriki na Croatia.

Uamuzi wa nani atacheza dhidi ya nani utafanywa baada ya orodha ya viwango vya soka duniani ya Fifa kutangazwa wiki ijayo.

Mada zinazohusiana