Batambuze mchezaji bora wa Septemba Tanzania

Shafik Batambuze aibuka mchezaji bora wa mwezi Septemba Tanzania Haki miliki ya picha Google
Image caption Shafik Batambuze aibuka mchezaji bora wa mwezi Septemba Tanzania

Mchezaji wa timu ya Singida United, Shafik Batambuze amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Septemba wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2017/2018.

Batambuze anayecheza nafasi ya ulinzi wa pembeni, alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda Ibrahim Ajibu wa Yanga na kiungo Mohammed Issa wa Mtibwa Sugar, alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam.

Uchambuzi huo kwa mujibu wa utaratibu hufanywa na kikao cha Kamati ya Tuzo ya VPL inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha waliopo viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu huu.

Mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa Singida United kupata pointi 10 katika michezo minne, ambayo timu yake ilicheza kwa mwezi Septemba.

Wadhamini wa ligi kuu ya Tanzania bara wana utaratibu wa kuwazawadia wachezaji bora wa kila mwezi,