Juan Mata awaomba wachezaji EPL wachange pesa

Juan Mata Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Juan Mata amechezea Uhispania mechi 41

Juan Mata amewaomba wachezaji wenzake Ligi Kuu ya England watoe ahadi sawa na yake ya kutoa mchango wa asilimia moja ya mshahara wao kwa hisani kusaidia watu wasiojiweza au makundi yanayosaidia watu wasiojiweza.

Wachezaji sota kufikia sasa wamekubali wito kwa kiungo huyo wa kati wa miaka 29 lakini hakuna mchezaji hata mmoja kutoka Ligi ya Premia hama mzaliwa wa Uingereza ameahidi kushiriki.

Mata amesema anatumai wachezaji wenzake, hasa Manchester United watajiunga naye karibuni.

Mhispania huyo alijiunga na United kutoka Chelsea kwa £37.1m mwaka 2014, na hulipwa takriban £7m kila mwaka.

Beki wa Ujerumani na Bayern Munich Mats Hummels alikuwa mchezaji wa kwanza kutikia wito kwa Mata wa kutoa 1% ya mshahara wake kwa hisani.

Washindi wa Kombe la Dunia la wanawake kutoka Marekani Megan Rapinoe na Alex Morgan, nyota wa Juventus Giorgio Chiellini, winga wa zamani wa Arsenal Serge Gnabry na mchezaji wa Stuttgart Dennis Aogo walifuata.

Mada zinazohusiana