Liverpool yatoka sare na Man United

Kipa David De Gea amefanikiwa kutofungwa katika mechi 18 za ligi ya Uingereza Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kipa David De Gea amefanikiwa kutofungwa katika mechi 18 za ligi ya Uingereza

Liverpool walizuiwa na kupata sare ya 0-0 licha ya kutawala mechi dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Anfield na sasa wameshinda mara moja kati ya mechi nane.

Kikosi hicho cha Jurgen Klopp kilikuwa juu kwa muda mrefu na kilishambulia lango la United mara 19 lakini kipa David De Gea alikuwa imara na kuwazuia.

United ilionekana kuzembea katika safu ya mshambulizi ijapokuwa Simon Mignolet alilazimika kulipangua shambulizi lililotekelezwa na Romelu Lukaku kabla ya muda wa mapumziko.

Liverpool iliendelea kutawala katika kipindi cha pili lakini Emre Can alipoteza fursa nzuri alipopiga juu ya goli akiwa yuiko umbali wa maguu manane pekee na goli .

Mada zinazohusiana