Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 04.12.2017

Thibaut Courtois Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Thibaut Courtois

Meneja wa Everton Sam Allardyce amemfanya mshambuliaji wa Watford Troy Deeney, 29, kuwa wa kwanza katika orodha yake wakati wa uhamisho wa mwezi Januari. (ESPN)

Meneja Antonio Conte ameiambia bodi ya Chelsea kushugulikia mikataba ya kipa Thibaut Courtois, 25, na mchezaji wa safu ya kati Eden Hazard, 26, kabla ya kuelekea kwa kombe la dunia wakichezea Ubelgiji. (Express)

Arsenal wako makini kumsaini mchezaji wa kiungo cha kati wa Sevilla Steven N'Zonzi, 28 baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Blackburn na Stoke kukosana na meneja wake Eduardo Berizzo. (AS, via Sun)

Image caption Steven N'Zonzi

Mshambuliaji wa Newcastle Aleksandar Mitrovic, 23, atarejea Anderlecht mwezi Januari wakati mahangaiko kwenye klabu hiyo yakiendelea

Everton, West Ham na Swansea wanarajiwa kungangania kumwinda mlinzi wa Augsburg Daniel Opare, 27, in January. (Mail)

Arsenal na Tottenham wana nia wa kumsaini Dani Ceballos. Mchezaji huyo wa kiungo cha kati mwenye umri wa miaka 21 hana furaha huko Real Madrid. (Calciomercato)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Dani Ceballos

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Schalke na Germany Leon Goretzka, 22, ataiambia Manchester United, Arsenal na Barcelona mipango yake ya siku za usoni mwishoni mwa Januari licha ya klabua hizo zote kummezea mate

Tottenham wanajiandaa kumpa ofa mchezaji wa kiungo cha kati Yusuf Yazici, anayekichezea klabu ya Uturuki cha Trabzonspor. (Sporx - in Turkish)

Klabu ya Gremio ya Brazil kimewaambia Barcelona kuwa watahitajika kulipa euro milioni 50 kumsaini mchezaji wa safu ya kati Arthur (RAC1, via Mail)

Mada zinazohusiana