Conte: Itabidi tujitahidi dhidi ya Southampton nusu fainali FA

Mkufunzi wa Chelea Antonio Conte
Image caption Mkufunzi wa Chelea Antonio Conte

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anasema kuwa Chelsea lazima iwe tayari kujikaza katika mechi ya nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Southampton.

The Blues ambao ndio mabingwa watetezi wa ligi ya Uingereza ,watakabiliana na Southampton siku ya Jumapili.

Conte ambaye kikosi chake kiliishinda Burnley 2-1 ugenini katika ligi ya Uingereza siku ya Alhamisi alisema kuwa hatowasikiza wale wanaosema kwamba Chelsea tayari imejikatia tiketi ya fainali ya kombe la FA.

''Haitakuwa rahisi'', alisema Conte, ambaye alisema kwamba huenda akaanza na washambuliaji wawili katika mechi hiyo.

''Siku tano zilizokwisha tulikuwa nyuma 2-0 dhidi ya Southampton ,lakini niliona ishara nzuri dhidi ya Burnley''.

Image caption Olivier Giroud

''Lazima tuendelee hivi. Katika mechi dhidi ya Burnley, Conte aliwachezesha washambuliaji wawili Alvaro Morata na Olivier Giroud kwa mara ya kwanza tangu achukue hatamu katika klabu hiyo 2016''.

''Awali ilikuwa vigumu kwangu mimi kuanza na washambuliaji wote wawili'', Alisema. ''lakini walionyesha uhusiano mzuri na wakati huohuo wakajitahidi sana''.

''Washambuliaji wetu waliwasumbua sana mabeki na tukaishangaza Burnley''.

''Ni mpango ambao ninaweza kuutumia siku ya Jumapili ama hata katika siku za usoni''.

Image caption Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata

Raia wa Uhispania Morata , ambaye alikosa fursa ya wazi ya nipe nikupe na kusalia na kipa alikasirika alipotolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Eden Hazard dakika 19 kabla ya mechi kukamilika.

''Lazima Alvaro amekasirika'', alisema Conte. ''Alikuwa na fursa ya kufunga na unapofunga unabadilisha imani ya timu''.

''Nilidhani alikasirishwa na kutolewa baada ya kushindwa kufunga lakini alinifurahisha sana''.

Image caption Eden Hazard

''Niliona ni vyema kuleta nguvu mpya kupitia Hazard.Chelsea ilipoteza 2-1 kwa Arsenal katika kombe la FA msimu uliopita.Sio jukumu langu kuzungumzia msimu huu jukumulangu ni kufanya jitihada na kuleta mafanikio katika timu''.

''Mara nyengine mimi ni mbaya na mara nyengine sio mzuri sana''."kuwaona Giroud na Morata wakicheza walivyocheza inaniridhisha sana.

Mada zinazohusiana