Tetesi za soka Ulaya Jumatano 09.05.2018

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger
Image caption Meneja wa Arsenal Arsene Wenger

Mkufunzi Arsene Wenger amesema kuwa huenda akachukua wadhfa wa afisa mkuu katika klabu ya Ufaransa ya PSG wakati atakapoondoka Arsenal mwisho wa msimu huu . (Telegraph)

Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney, 32, yuko katika mazungumzo na klabu ya ligi ya Marekani D.C United kuhusu uhamisho wa mwisho msimu huu .[Washington Post)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wayne Rooney

Lakini itahitaji ombi kubwa kutoka China ama Marekani kwa nahodha huyo wa zamani wa Uingereza kuondoka Everton mwisho wa msimu huu kulingana na mkufunzi Sam Allardyce. (Liverpool Echo)

Manchester United imejiandaa kumshirikisha mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 22, katika makubaliano na klabu ya Borussia Dortmund na winga wa Marekani Christian Pulisic, 19. (Mirror)

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri

Mkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri anasema kuwa atafanya mazungumzo na klabu hiyo ya Itali mwisho wa msimu huu huku kukiwa na madai kwamba huenda akajiunga na Arsenal msimu ujao. (Express)

Wachezaji wa Arsenal wanaendelea kukatishwa tamaa baada ya kiungo wa kati Mesut Ozil 29 kupata jereha litakalomweka nje kwa kipindi chote kilichosalia cha msimu huu. (Mail)

Everton, Burnley na Wolvehampton ni miongoni mwa klabu za ligi ya Premia msimu ujao zinazomnyatia kiungo wa kati wa Manchester City Yaya Toure, 34, mwisho wa msimu huu. (Mirror)

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mesut Ozil wa Arsenal

Juventus bado haijawasilisha ombi la mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata, 25, licha ya ripoti kwamba kuna makubaliano kuhusu kitita fulani. (Goal)

Wolves wanataka kumsajili mshambuiaji wa AC Milan na Ureno Andre Silva, 22, msimu huu. (Sky Sport Italia)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alvaro Morata

Newcastle haina haja ya kumsajili mshambuliaji wa Leicester na Algeria Islam Slimani, 29, kwa mkataba wa kudumu msimu huu kufuatia uhamisho wake wa mkopo.(Chronicle)

Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anasema kuwa klabu hiyo italazimika kuvunja rekodi yao ya uhamisho ya dau la £16m alilopewa Michael Owen mwaka 2005 - iwapo italazimika kumsajili mshambuliaji kufunga mabao mengi msimu ujao. (Mail)

Image caption Antoine Griezman

Atletico Madrid inataka mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann kusalia katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu na tayari rais wa klabu hiyo Enrique Cerezo amekutana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 katika mgahawa mmoja mjini Madrid ili kumshawishi kusalia . (AS - in Spanish)

Pep Guardiola amekataa kuandikisha mkataba wa kudumu na klabu ya Manchester City . (Star)

Kiungo wa kati wa zamani wa Itali Andrea Pirlo ana hamu ya kuanza kuwa mkufunzi na amekiri kwamba angependelea kufanya kazi na timu ya taifa ya Italii. (Sky Sports)

Mada zinazohusiana