Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 10.05.2018

Neymar Jr
Image caption Neymar Jr

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar , 26, alifanya mazungumzo ya siri na Real Madrid mnamo mwezi Machi. Mchezaji huyo wa Brazil amedaiwa kutaka kuondoka mjiini Paris(AS, via Express).

Mabingwa wapya wa ligi ya mabingwa Wolvehampton ambao wamepandishwa daraja katika ligi kuu ya Uingereza ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu kumsaini mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney, 32, mwisho wa msimu huu(Birmingham Mail)

Image caption Wayne Rooney

Lakini Rooney hatatoa uamuzi wa iwapo atasalia katika uwanja wa Goodison Park hadi pale hatma ya mkufunzi Sam Allardyce itakapoamuliwa(Star).

Klabu ya ligi ya Marekani ya DC United ina matumaini kwamba inaweza kumshawishi mfungaji huyo wa mabao mengi nchini Uingereza kujiunga nao(Washington Post) .

Image caption Jack Wilshere amepatiwa mkataba wa miaka mitatu na Arsenal

Arsenal imempatia kiungo wa kati Jack Wilshere, 26, mkataba mpya wa miaka mitatu ikiwemo kuongeza mkataba huo kwa miezi 12 na hivyobasi kumzuia mchezaji huyo katika uwanja wa Emirates hadi 2022. (Mirror)

The Gunners wameanza mazungumzo ya kumsajili kipa wa Bayer Leverkusen Bernd Leno, 26, kuchukua mahala pake Petr Cech. (Bild, via Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption PSG itashindana na Tottenham katika kumsaini beki na kinda wa Fulham Ryan Sessegnon,

PSG itashindana na Tottenham katika kumsaini beki na kinda wa Fulham Ryan Sessegnon, huku mchezaji huyo wa Uingereza akitarajiwa kuwa na thamani ya £50m. (Mirror)

Southampton inapanga kuanza mazungumzo wiki ijayo na mkufunzi Mark Hughes kuhusu mkataba wa kudumu wa miaka mitatu huku watakatifu hao wakiwa katika hali ya kujinusuru kushiriki katika ligi ya Uingereza.(Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Roma imejianda kuzishinda timu kadhaa za Uingereza katika usajili wa mshambuliaji wa Uholanzi na Ajax ,19,Justin Kluivert. (Vl.nl, via Talksport)

Roma imejianda kuzishinda timu kadhaa za Uingereza katika usajili wa mshambuliaji wa Uholanzi na Ajax ,19,Justin Kluivert. (Vl.nl, via Talksport)

Mchezaji anayelengwa na Tottenham Matthijs de Ligt, 18, anataka kuondoka Ajax, huku beki huyo wa Uholanzi akihusishwa na Bayern Munich pamoja na Barcelona. (De Telegraaf, via Talksport)

Leicester, Newcastle na Watford zinamtaka mshambuliaji wa Hannover mwenye umri wa miaka 25 Niclas Fullkrug. (Leicester Mercury)

Liverpool inaongoza mkondo katika kumsajili mchezaji wa Porto's Diogo Leite mwisho wa msimu huu huku beki huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 19 pia akinyatiwa na Manchester City na Arsenal. (Guardian)

Image caption Newcastle na Celtic zinamnyatia beki wa West Brom, 28, Craig Dawson,

Newcastle na Celtic zinamnyatia beki wa West Brom, 28, Craig Dawson, huku raia huyo wa Uingereza akiwa na thamani ya £15m. (Mail)

Matumaini ya kiungo wa kati wa Norwich City na Uingereza James Maddison kujiunga na ligi kuu ya Uingereza yamepigwa jeki kufuatia habari kwamba hana jereha baya la goti kama ilivyodhaniwa awali - Manchester City, Tottenham, Arsenal na Everton ni miongoni mwa klabu zinazommezea mate mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Mirror)

Chelsea inapanga kufutilia mbali mkopo wa Charly Musonda wa miezi 18 kutoka Celtic na kumpeleka raia hyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 21 katika klabu nyengine msimu ujao (ESPN)

Shabiki wa Arsenal amekataa ombi la £1,000 kwa tai ya mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger aliyompatia mwanawe wa miaka saba. (Sun)

Mada zinazohusiana