Ngorongoro Heroes wa Tanzania wacharazwa 2-1 ugenini Mali

timu ya under 20 Haki miliki ya picha Google
Image caption Timu ya Ngorongoro Heroes ya Tanzania

Tanzania imejiweka kwenye mazingira magumu ya kusonga mbele katika mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Vijana chini ya umri wa miaka 20 Afrika, baada ya kufungwa mabao 2-1 na timu kutoka nchini Mali mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Tanzania, Ngorongoro Heroes sasa watalazimika kwenda kushinda ugenini kuanzia 2-0 Mei 20 mjini Bamakonchini Mali, katika mchezo wa marudiano ili kuingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya Niger mwakani.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa kutoka Comoro, Soulaimane Ansudane aliyepuliza kipyenga akisaidiwa na washika vibendera Mmadi Faissoil na Abdoulmadjid Azilani, hadi mapumziko tayari Mali walikuwa mbele kwa mabao 2-1.

Ousmane Diakite alianza kuifungia Mali dakika ya 37 akitumia makosa ya kipa wa Ngorongoro Heroes, Abdultwali Msheri kupiga mpira bila uangalifu, ambao ulinaswa na wapinzani na kufunga.

Wakati Ngorongoro Heroes wanahangaika kutafuta bao la kusawazisha, wakajikuta wakichapwa bao la pili kirahisi kwa makosa ya kipa tena, mfungaji Samadiare Dianka kwa shuti la mpira wa adhabu.

Msheri alikwenda kusimama nyuma ya ukuta wa wachezaji wake na kumrahisishia Dianka kazi kwa kuupeleka mpira upande uliokuwa wazi, kushoto kwa mlinda mlango huyo.

Mshambuliaji chipukizi wa Azam FC, Paul Peter akaifungia Ngorongoro Heroes bao la kufutia machozi dakika ya 44 akiuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Mali, Youssouf Keita kufuatia shuti la mpira wa adhabu.

Kipindi cha pili mvua iliyoanza kunyesha tangu asubuhi ikaongezeka na ladha ya mpira ikapungua kutokana na uwanja kuwa unateleza na haikuwa ajabu matokeo hayakubadilika.

Kipigo cha leo lawama zinakwenda kwa Kocha Mkuu, Ammy Ninje ambaye hakumpanga kipa namba moja, Ramadhani Kabwili ambaye alitofautiana naye kabla ya mchezo .

Mada zinazohusiana