City kuiomba Birmingham

Manchester City imefanya mazungumzo na Birmingham City kuhusu uwezekano wa kumchukua tena golikipa Joe Hart, aliyeko huko kwa mkopo.

Golikipa namba moja wa Man City Shay Givenhatoweza kucheza michezo iliyosalia ya msimu huu baada ya kutenguka bega, katika mchezo waliotoka sare na Arsenal siku ya Jumamosi.

Kipa mwingine wa akiba wa City, Stuart Taylor pia ni majeruhi, na hivyo kusalia Gunnar Nielsen ambaye hana uzoefu mkubwa.

Hata hivyo, Birmingham kwa mujibu wa mkataba, hawalazimiki kumrejesha kipa huyo.

Iwapo Birmingham itakubali kumruhusu arejee City, italazimu mkataba hatua hiyo kuridhiwa na Chama cha Soka cha England, FA, huku vilabu vingine huenda vikapinga jambo hilo.

Manchester City, iliyo katika nafasi ya sita, pamoja na Aston Villa, Tottenham na Liverpool, zote zinawania nafasi ya nne, ambayo huja na kitita cha mamilioni ya dola kutokana na kushirkiki katika michuano ya klabu bingwa Ulaya.

Wasemaji wa Villa, Spurs na Liverpool wote wamesema 'hawana la kusema' kuhusuana na uamuzi wa FA.

Pointi mbili tu ndio tofauti kati ya timu hizo.