Historia ya Ligi kuu ya England

Historia ya Premier League

Ligi Kuu ya soka ya England ndiyo yenye kutazamwa na watu wengi zaidi kuliko yoyote ile duniani. Ndiyo tajiri zaidi kulizo zote ikiwa imeweza kuvutia wachezaji bora kutoka kila pembe ya dunia. Lakini ni ngumu kuamini kwamba mpira wa kwanza kupigwa katika Ligi Kuu ya Premier ilikuwa hivi karibuni tu 15 mwezi wa Nane 1992.

Image caption Soka ni mchezo unaopendwa sana

Kipindi cha miaka ya 1980 kilikuwa kigumu kwa soka ya England. Uhuni katika viwanja vingi vya soka ulishamiri. Timu za soka za England zilipigwa marufuku katika miuchuano ya Ulaya kufuatia vifo vya mashabiki 39 katika uwanja wa Heysel nchini Ubelgiji kabla ya pambano la fainali ya kombe la Ulaya kati ya Liverpool na Juventus mwaka 1985. Ni wachezaji wachache bora duniani wangeweza hata kufikiria kucheza soka la kulipwa England.

Ndipo mwaka 1989 ikatoka ripoti ya Hillsborough and the Taylor. Washabiki wa soka 96 walifariki na wengine 150 walijeruhiwa katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Chama cha Soka England (FA) kati ya Liverpool na Nottingham Forest. Ripoti ya Lord Taylor ikapendekeza kubadilishwa kabisa mfumo wa uendeshaji wa viwanja vya soka na kusababishwa kuanzishwa kwa utaratibu wa kukaa vitini kwa watazamaji wote wa soka wawapo viwanjani.

Mabadiliko makubwa ya muundo

Gharama kubwa za kutekeleza mapendekezo ya tume na hali ya kutoweza kuvutia wachezaji bora wa kulipwa ikasababisha vilabu vikubwa kuonesha hali ya kurodhia. Mapema mwaka 1988, vilabu kumi vilitishia kujitoa kutoka Ligi Kuu ili vifaidi mapato makubwa yatokanayo na matangazo ya runinga.

Image caption Nembo ya Ligi kuu ya England

Hakika badiliko kubwa la muundo lilikuwa linahitajika ikiwa klabu za England na mchezo wenyewe wa soka vilihitaji kustawi. Makubaliano ya wanachama waanzilishi yakasainiwa 17 mwezi wa Saba 1991 na kuweka kanuni za msingi za kuanzisha Ligi Kuu ya Soka. Ligi hiyo ingekuwa na uhuru wa kibiashara toka kwa Ligi ya Soka na Chama cha Soka (FA), ikiwa na mamlaka ya kuratibu mikataba yake yenyewe ya utangazaji na udhamini wa soka.

Tarehe 20 mwezi wa Pili 1992 klabu za ligi daraja la kwanza zikang’atuka toka Ligi ya Soka kwa pamoja na miezi mitatu baadae Ligi Kuu ya soka (Premier League) ikaanzishwa kama kampuni (limited company).

Ligi hiyo ikaamua kuchukua hatua kubwa kwa kuto haki za matangazo ya runinga kwa kituo cha Sky TV. Wakati huo kutoza wapenzi wa soka gharama za kutazama soka ilikuwa ni dhana mpya. Lakini ubora wa soka uliotarajiwa kupatikana na mikakati mizito ya kutafuta soko ya kituo cha Sky vikasababisha thamani ya Ligi ya Premier kukua. Makubaliano ya mwanzo yalikuwa kiasi cha pound milioni 191 kwa kipindi cha miaka mitano.Kutangaza mechi za soka kutoka 2007-2010 Sky na Setanta wamelipa kiasi cha pound bilioni 1.7!!

Udhamini pia umeweza kuwa na mchango mkubwa. Mwaka 1993 Carling ililipa pound milioni 12 kwa kipindi cha miaka minne na mashindano yakajulikana kama FA Carling Premiership. Wakaongeza mkataba kwa miaka mingine minne kwa ongezeko la asilimia 300. Mwaka 2001, Barclaycard wakawa ndiyo wadhamini wapya na kutoa kiasi cha pound milioni 48 kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu. Barclays wakachukua udhamini mwaka 2004 na mwaka 2007 wakaongeza bei kufikia pound milioni 65 kwa misimu mitatu.

Image caption Kocha wa Liverpool, Rafael Benitez

Kuongezeka kwa mapato kumehakikisha kuwa timu za England zinaweza kushindana katika ngazi ya dunia juu ya suala la ada za uhamisho wa wachezaji na mishahara yao. Hii ni sababu kubwa ambayo imefanya baadhi ya wachezaji wakubwa duniani kuing’arisha Barclays Premier League.

Mwaka 1992 kulikuwa na wachezaji 11 tu wasiokuwa waingereza au wa-Irish katika Premier League. Kufikia 2007, idadi ikaongezeka na kufikia 250. Katika miaka yote hii wachezaji toka nje ya Uingereza wamechangia kuing’arisha soka ya Uingereza. Makocha (meneja) kutoka nje pia wamekuwa pia na shauku ya kufanya kazi England. Mbinu za ufundishaji wa soka za makocha kama Arsene Wenger, Gerrard Houllier na Ruud Gullit hakika zimekuwa na mchango mkubwa.

Ligi Kuu ya soka England (Premier League) mwanzoni ilikuwa na klabu 22 lakini kukawepo na nia ya kutaka kupunguza idadi hadi 20 ili kuleta ustawi zaidi na ubora katika ngazi ya klabu na kimataifa. Hii nia ikafanikiwa mwishoni mwa msimu wa 1994/95 wakati vilabu vinne viliposhushwa daraja na na viwili kupandishwa.

Timu ya Burnley ikapanda daraja mwaka 2009 na kufikisha idadi ya timu ambazo zimewahi kushiriki Premier League kufikia 43. Timu yenye mafanikio kuliko zote katika historia ya Premier League bila ya shaka ni Manchester United. Ikiongozwa na Sir Alex Ferguson imeweza kunyakua mataji 11 na haijatokea ikamaliza ligi ikiwa katika nafasi chini ya tatu tangu kuanzishwa kwa Premier League mwaka 1992