Fulham kidedea, kucheza fainali Europa

Fulham na Wolfsburg
Image caption Mpambano wa Fulham na Wolfsburg.

Fulham wameandika historia walipojikwamua na kufanikiwa kuitandika Hamburg kuingia fainali ya ligi ya soka ya Europa kwenye mechi iliyofanyika Craven Cottage, uwanja wa Fulham.

Ndoto ya kocha Roy Hodgson kuiongoza Fulham kucheza fainali yao ya kwanza barani Ulaya ilitimia, ingawa mechi ilianza vibaya kwao baada ya mkwaju wa adhabu uliopigwa maridadi na Mladen Petric uliwapatia Hamburg goli la kuongoza.

Hamburg, wakicheza kwa kutambua fainali itachezwa kwenye uwanja wao wa Nordbank Arena, walidhibiti vyema dakika 60 za kwanza za mechi hiyo - lakini kama walivyofanya katika mechi zilizotangulia barani Ulaya, Fulham walijibu mashambulizi na kuwalemea Wolfsburg kutoka Ujerumani.

Fulham walimudu kupata ushindi katika kipindi cha pili licha ya kumkosa mfungaji wao bora Bobby Zamora, ambaye bado anasumbuliwa na majeraha.

Wenyeji walipata magoli yao kupitia Simon Davies kunako dakika ya 69 na Zoltan Gera aliandika la pili la kuamsha nderemo kwa mashabiki wa Fulham wakisherehekea mafanikio ya kihistoria.