Benitez ataka mabadiliko Liverpool

Meneja wa Liverpool Rafael Benitez amekiri kuwa itamlazimu asajili wachezaji wapya kadhaa ili kurejea kuwa timu kali tena.

Image caption Rafael Benitez amesema kuna kazi kubwa ya kufanya

Liverpool walitolewa na Atletico Madrid kwa sheria ya goli la ugenini katika nusu fainali ya ligi ya Europa na kufuta kabisa matumaini ya kumaliza msimu na kombe lolote.

Hata hivyo Liverpool bado wana nafasi ya kumaliza katika nafasi ya nne ili kuweza kucheza ligi ya klabu bingwa Ulaya, ingawa nafasi yenyewe ni finyu.

Watahitaji kupata ushindi dhidi ya Chelsea siku ya Jumapili.

Benitez amekiri kuwa kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuirejesha Liverpool katika enzi zake za kutamba katika soka.