Algeria yataja kikosi chake - Kombe la Dunia

Algeria imetaja kikosi kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia.

Image caption Wachezaji wa Algeria wakishangilia kufuzu Kombe la Dunia

Kikosi hicho ni pamoja na Nedir Belhadj na Faouzi Chaouchi ambao wametajwa katika kikosi cha awali licha ya kuwa wawili hao huenda wasicheze michezo kadhaa kutokana na adhabu.

Wawili hao walipewa kadi nyekundu katika nusu ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Januari mwaka huu na kupewa adhabu.

Belhadj ambaye ni beki wa Portsmouth ya England pamoja na golikipa namba moja Chaouchi watakosa mchezo wa ufunguzi dhidi ya Slovenia. Chaouchi pia atakosa mchezo dhidi ya England.

Wachezaji wengine katika kikosi cha Algeria wako Marekani.

"Imekuwa kazi ngumu kuchagua, lakini nilitaka kuweka kikosi kilichocheza Kombe la Mataifa hadi nusu fainali nchini Angola" amesema kocha Rabah Saadane.

Wachezaji wengine watano wataogenzwa Mei 11, siku mbili kabla ya kikosi hicho kukutana Crans-Montana, nchini Uswisi kwa ajili ya mazoezi yao ya kwanza kabisa.

Image caption Kikosi cha Algeria chatajwa

Mchezaji mwingine ambaye atakuwa akitumaini kuitwa ni minga wa klabu ya Blackpool hameur Bouazza, ambaye amekuwa akisumbuliwa na nyonga katika wiki za hivi karibuni.

Kuna wachezaji wanne pekee wasiocheza soka la kimataifa, katika kikosi hicho, ambapo watatu kati yao ni magolikipa.

Baada ya kufanya mazoezi katika kambi yao nchini Uswisi, mabweha hao wa jangwani watapambana na Jamhuri ya Ireland katika mchezo wa kirafiki tarehe 28 Mei, halafu watapambana na Falme za Kiarabu na Ujerumani wiki moja baadaye.

Image caption Mashabiki wa Algeria

Kikosi hicho ni kama ifuatavyo na vilabu wanavyochezea katika mabano:

Magolikipa:Lounes Gaouaoui (ASO Chlef), Faouzi Chaouchi (Entente Setif), Mohamed Lamine Zemmamouche (MC Alger), M'bohi Rais Ouheb (Slavia Sofia, Bulgaria)

Mabeki: Abdelkader Laifaoui (Entente Setif), Madjid Bougherra (Rangers, Scotland), Carl Medjani (Ajaccio, France), Rafik Halliche (Nacional Madeira, Portugal), Anther Yahia (Bochum, Germany), Habib Belaid (Boulogne-sur-Mer, France), Nadir Belhadj (Portsmouth, England), Djamel Mesbah (Lecce, Italy)

Viungo: Hassan Yebda (Portsmouth, England), Medhi Lacen (Racing Santander, Spain), Yazid Mansouri (Lorient, France), Adlene Guedioura (on loan at Wolverhampton, England from Charleroi, Belgium), Riad Boudebouz (Sochaux, France), Djamel Abdoun (Nantes, France), Fouad Kadir (Valenciennes, France), Mourad Meghni (Lazio, Italy), Karim Ziani (Wolfsburg, Germany), Karim Matmour (Borussia Moenchengladbach, Germany)

Washambuliaji: Abdelkader Ghezzal (Siena, Italy), Rafik Djebbour (AEK Athens, Greece), Rafik Saifi (Istres, France)