Tottenham kucheza ligi ya mabingwa Ulaya

Tottenham Hotspur imejihakikishia kucheza ligi ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao, baada ya kuinyuka Manchester City kwa goli 1-0.

Image caption Goli pekee la Peter Crouch limeipeleka Spurs kucheza 'Ulaya'

Goli pekee lililofungwa na Peter Crouch katika kipindi cha pili, limethibitisha klabu hiyo ya Kaskazini mwa London inajikita katika nafasi ya nne.

Spurs sasa imefikisha pointi 70 huku mchezo mmoja tu ukisalia kumaliza ligi kuu ya England. City wenye pointi 66 ilitakiwa kupata ushindi dhidi ya Spurs ili kuweka matumaini ya kumaliza katika nafasi ya nne.

Timu zinazocheza katika ligi ya mabingwa Ulaya hupata kitita kinono kutoka katika shirikisho la soka la Ulaya, Uefa.