Argentina yamuacha Cambiasso

Wachezaji wawili wa Inter Milan Esteban Cambiasso na Javier Zanetti wameachwa katika kikosi cha wachezaji wa awali wa Argentina kitakachojimwaga katika Kombe la Dunia.

Image caption Diego Maradona

Mlinzi Zanetti na kiungo Cambiasso wameondolewa katika kikosi cha Argentina licha ya kuwa nguzo walipoiwezesha Inter kuingia hatua ya nusu fainali ya Ubingwa wa Ulaya.

Kocha Diego Maradona amewajumuisha katika kikosi chake Maxi Rodriguez wa Liverpool na Fabricio Coloccini anayechezea New Castle.

Maradona atapunguza kikosi chake hicho na kubakiwa na wachezaji 23 itakapofika tarehe 1 Juni.

Kuna jumla ya wachezaji watano wanaocheza soka England katika kikosi hicho cha Argentina, akiwemo Carlos Tevez wa Manchester City, kiungo wa Newcastle Jonas Gutierrez na Javier Mascherano wa Liverpool.

Kikosi cha Argentina

Walinda Mlango: Sergio Romero (AZ Alkmaar), Mariano Andujar (Catania), Diego Pozo (Colon)

Walinzi: Nicolas Burdisso (Inter Milan), Martin Demichelis (Bayern Munich), Walter Samuel (Inter Milan), Gabriel Heinze (Olympique Marseille), Nicolas Otamendi (Velez Sarsfield), Fabricio Coloccini (Newcastle), Juan Manuel Insaurralde (Newell's Old Boys), Clemente Rodriguez (Estudiantes), Ariel Garce (Colon)

Wachezaji wa Kiungo: Javier Mascherano (Liverpool), Sebastian Blanco (Lanus), Juan Sebastian Veron (Estudiantes), Jesus Datolo (Olympiacos), Jose Sosa (Estudiantes), Maximiliano Rodriguez (Liverpool), Mario Bolatti (Fiorentina), Juan Mercier (Argentinos Juniors), Angel Di Maria (Benfica), Jonas Gutierrez (Newcastle), Javier Pastore (Palermo)

Washambuliaji: Sergio Aguero (Atletico Madrid), Diego Milito (Inter Milan), Martin Palermo (Boca Juniors), Carlos Tevez (Manchester City), Gonzalo Higuain (Real Madrid), Lionel Messi(Barcelona), Ezequiel Lavezzi(Napoli)