England yashinda Cricket Twenty20

Nahodha wa timu ya taifa ya Kriketi ya England Paul Collingwood amesema ubingwa wa dunia ilioupata nchi yake wa mashindano ya Twenty20 umeonesha ushindani uliokuwepo mwaka 2005 na 2009 wakati wa mfululizo wa mashindano ya Ashes Test dhidi ya Australia.

Image caption Paul Collingwood

England iliifunga Australia kwa wiket saba katika mchezo wa mwisho siku ya Jumamosi huko Barbados na kuweza kujihakikishia taji lao la kwanza la ushindi wa dunia kwa mchezo wa siku moja.

Amesema: "Ni jambo zuri kuwa hapa tulipofika. Huu ni ushindi wetu wa kwanza wa Taji la Dunia kuweza kushinda na vijana walistahili kushinda.

"Tulifanya kazi ya ziada na jitahada kubwa na vijana kwa kweli walichachamaa kufanikisha ubingwa."

England imewahi kusindwa katika fainali nne za historia ya miaka 35 ya mashindano ya siku moja ya kimataifa, lakini siku ya Jumapili mara kwa mara ilikuwa inapewa nafasi ya kushinda baada ya kuiweka nyuma Australia kwa 8-3.