12 Juni, 2010 - Imetolewa 16:17 GMT

Marekani yaipania England

Capello ana kibarua kizito kuijengea England mafanikio katika Kombe la Dunia.

Mamilioni ya mashabiki wa England wana shauku ya mechi ya kwanza katika Kombe la Dunia 2010, mpambano ni dhidi ya Marekani.

Chama cha wauza bia na wamiliki wa maduka ya vinjwaji wamesema takriban mashabiki milioni nne wanatarajiwa katika baa na skrini kubwa zilizowekwa maeneo ya wazi kuangalia shughuli hiyo.

Katika ujumbe wa video kuwaunga mkono wachezaji wake, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron alisema: "Come on England".

Kuona matokeo live na msimamo wa makundi unatakiwa kuwezesha javascript.

Mechi hiyo inacheza Rustenburg, South Africa, na itaanza saa tatu na nusu za Afrika Mashariki.

Meneja wa England, Fabio Capello amesema asingetaja wachezaji wake mapema katika mechi hiyo.

Uhasama unatarajiwa kuwa mkubwa katika mechi hiyo, huku Marekani ikijaribu kuiangusha England.

BBC navigation

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.