13 Juni, 2010 - Imetolewa 13:54 GMT

Ghana vitani na Serbia

Ghana imekuwa timu ya kwanza ya Afrika kupata ushindi katika mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini Afrika Kusini baada ya kuitandika Serbia 1-0.

Goli hilo pekee lilifungwa na Asamoah Gyan kwa njia ya penati baada ya Zdravko Kuzmanović kuunawa mkono ndani ya sanduku la 18.

Awali, Aleksandar Luković, alitolewa nje baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.

Mpambano huo ulikuwa muhimu kwa Ghana, hasa baada ya Nigeria na Algeria kufungwa mechi za kwanza. Afrika Kusini ilitoka sare ya 1-1 katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Mexico.

Jedwali hapo chini linakupa maelezo yote ya mechi kadri ilivyokuwa ikiendelea uwanjani. Mfano mfungaji wa goli na muda aliofunga, kadi na takwimu nyingine.

Kuona matokeo live na msimamo wa makundi unatakiwa kuwezesha javascript.

BBC navigation

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.