25 Juni, 2010 - Imetolewa 17:59 GMT

Marekani na Ghana

Ushindi wa magoli 2-1 ulitosha kuipatia Ghana tiketi ya kucheza robo fainali kwa kuing'oa Marekani katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Royal Bafokeng.

Ghana walianza kupata goli kunako dakika ya tano, mfungaji akiwa Kevin-Prince Boateng.

Mpaka mapumziko, Ghana waliendelea kuwa mbele kwa goli hilo moja, Marekani walifanya mabadiliko kwa kumwingiza Benny Feilhaber aliyechukua nafasi ya Robbie Findley.

Landon Donovan aliisawazishia Marekani katika dakika ya 62, goli lililoipatia Marekani nguvu ya kuisumbua zaidi ngome ya Ghana.

Mpaka dakika 90, timu zote zilikuwa zimefungana 1-1. Ndipo mwamuzi Viktor Kassai alipoamuru dakika za nyongeza.

Katika muda wa nyongeza, Asamoah Gyan alifunga goli maridadi dakika ya tatu kipindi cha kwanza cha muda wa nyongeza.

Kwa matokeo hayo, Ghana watacheza dhidi ya Uruguay katika mpambano unaotarajiwa kuwa mkali.

Kuona matokeo live na msimamo wa makundi unatakiwa kuwezesha javascript.

BBC navigation

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.