Mo Farah awika katika riadha

Mo Farah
Image caption Mwanariadha wa Uingereza aliyezaliwa Mogadishu

Mwanariadha wa Uingereza, Mo Farah, na ambaye alizaliwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, amefanikiwa kushinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 10,000, mashindano ya riadha ya bara Ulaya, mjini Barcelona, Uhispania.

Mo Farah aliingia nchini Uingereza mwaka 1993 kama mkimbizi, na alikuwa hawezi hata kuzungumza Kiingereza kwa ufasaha.

Mwalimu wake wa mazoezi ya viungo mjini London, alikosomea, ndiye aliyegundua kipawa chake cha riadha.

Baada ya ushindi huo, alisema licha ya kujitahidi kadri ya uwezo wake wote miaka minne iliyopita, alishindwa kwa nusu-sekunde, na jambo ambalo limemkera mno, kusubiri kwa miaka minne kupata ushindi huo.