Gemma awika Hungary

Gemma Spofforth, kwa mara ya pili aliiwezesha Uingereza kuchukua nafasi ya kwanza na ya pili katika mashindano ya Ulaya ya kuogelea, mjini Budapest, Hungary.

Gemma alipata medali ya dhahabu katika mashindano ya mita 100 ya wanawake, ya kuogelea kwa mtindo wa backstroke.

Muogeleaji huyo mwenye umri wa miaka 22, aliweza kumzuia mwenzake wa Uingereza Lizzie Simmonds kupata ushindi.

Simmonds hatimaye alipata medali ya fedha.

Awali, katika mashindano ya Jumatatu, Lizzie alikuwa amepata medali ya dhahabu katika mashindano ya mita 200, kwa muda wa sekunde 59.80secs.

Liam Tancock alipata medali kwa fedha kwa mashindano ya wanaume ya mita 50 backstroke, huku Hannah Miley akipata medali ya shaba katika mashindano mengine ya wanawake ya mita 200.

Lakini licha ya Uingereza kung'ara katika mashindano hayo, Rebecca Adlington, anayeshikilia medali mbili za Olimpiki, ameomba radhi kwa kushindwa kufanya vyema katika mashindano ya Budapest.

Rebecca aliwaomba msamaha mashabiki wake, baada ya kumaliza katika nafasi ya saba, katika mashindano ya kina dada ya kuogelea mita 800, kwa kutumia mtindo wa freestyle.