14 Agosti, 2010 - Imetolewa 16:21 GMT

Liverpool na Arsenal

Mpambano kati ya Liverpool dhidi ya Arsenal utakaofanyika Anfield, umechochea ubishi kati ya mashabiki wa timu hizo mbili, nani atashinda kwa magoli mangapi? Roy Hodgson atakuwa akisimamia mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya Soka ya England tangu achukue hatamu kuifunza Liverpool.

Arsene Wenger hajafanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake kilichoambulia nafasi ya tatu, na ukame wa vikombe kwa miaka takriban mitano iliyopita, atakuwa na kazi ngumu ya kuhakikisha timu yake inaanza vizuri msimu mpya.

Idhaa ya Kiswahili ya BBC itatangaza mechi hiyo moja kwa moja, kama itakavyokuwa kwa mechi nyingine za Jumapili msimu huu zitakuwa zikipatikana moja kwa moja.

Kuona matokeo live na msimamo wa makundi unatakiwa kuwezesha javascript.

BBC navigation

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.