Schwarzer mbioni kwenda Arsenal?

Image caption Mark Schwarzer anawaniwa na Arsenal, lakini Fulham hawataki kumwuza bei ya kutupa.

Taarifa kutoka baadhi ya vyombo vya habari vya England zinaeleza kuwa Fulham itakubali kumwuza mlinda mlango Mark Schwarzer endapo Arsenal itakuwa tayari kumwachia mshambuliaji wake Carlos Vela juu ya fedha watakazokubaliana.

Mazungumzo ya timu hizo mbili za London yamekwama kwasababu Arsenal haipo tayari kulipa pauni milioni nne ambazo Fulham inataka kwa ajili ya kumwachia mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 37.

Awali Arsenal walitangaza kutaka kulipa pauni milioni mbili kumnunua Schwarzer mwezi Mei na hawajataja nyongeza tangu wakati huo, ingawa inaeleweka kuwa vilabu hivyo viwili bado vinaendelea na mazungumzo.