Arsenal yaitandika Bolton 4-1

Arsenal walisherehekea goli la 1000 tangu waanze kufundishwa na Arsene Wenger kwa ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya Bolton waliomaliza mechi wakiwa 10 uwanjani.

Laurent Koscielny aliipatia Arsenal goli la kuongoza katika dakika ya 24, lakini mlinzi huyo wa Ufaransa, alifanya kosa lililotoa fursa kwa Johan Elmander kusawazisha dakika moja kabla ya mapumziko.

Image caption Arsenal wameipa kipigo Bolton kusherehekea magoli 1000 tangu Arsene Wenger aanze kuifunza timu hiyo.

Lakini Arsenal walicharuka kwa Maroune Chamakh kufunga la pili kwa kichwa ndani ya miguu sita ya sanduku la Bolton.

Mlinzi Gary Cahill alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kufanya madhambi, kisha Alex Song na Carlos Vela wakakamilisha magoli mawili ya mwisho.

Licha ya kuwakosa Theo Walcott na Robin van Persie waliojeruhiwa, kikosi cha Wenger kilionekana kujitosheleza katika ushambuliaji..

Wafungaji

Arsenal 4-1 Bolton Mwisho
(Mapumziko 1-1)
Koscielny 24Chamakh 58A Song 78Vela 83 Elmander 44

Matokeo ya mechi nyingine

Fulham 2 - 1 Wolves

Man City 1 - 1 Blackburn

Newcastle 0 - 2 Blackpool

West Brom 1 - 1 Tottenham

West Ham 1 - 3 Chelsea

Wigan 1 - 1 Sunderland